Chiki anapanga harusi yetu, Bien wa Sauti Sol asema

Bien, mwanamziki wa kundi la Sauti Sol anatarijia kufunga ndoa na mchumba wake Chiki mwaka huu.

Akiongea na Word Is Ijumaa, alisema, ''Harusi itakuwa lakini kuhusu maendeleo yake, nimemwacha mchumba wangu kufanya mipangilio.''

Aliongeza, ''siwezi iepuka kwa kuwa nampenda kidosho huyu sana.''

Bien-Aime Baraza alimposa kidosho huyu, Chiki Kuruka, ambaye wamekuwa na mahusiano kwa muda mrefu, mwanzoni mwaka huu kwenye mazingira ya kuvutia sana.

Bien alienda chini kwa goti lake wakiwa Westgate Mall iliyo Nairobi, Kenya. Mwimbaji huyu tajika wa Africa alihakikisha kuwa sherehe hiyo ilikuwa yenye usiri. Alikodi chumba zima cha sinema na kuhakikisha kuwa ni rafiki zao wachache walishuhudia hafla hiyo.

''Awali nilikuwa nimewaambia baadhi ya watu wa familia yake na rafiki zake wachache wachukue video huku wakisema sababu wanampenda. Kila mmoja wao alikuwa na kitu kizuri cha kusema kumhusu, kisha nikatengeneza video kamili,'' Bien alisema katika mahojiano ya awali na Word Is.

Rafiki yake alimdanganya kuwa alikuwa na mzozo na mpenzi wake na alitaka awe hapo wakitatua shida zao. Baadae walikuwa waelekee  kuona sinema, mahali ambapo Bien na rafiki zake walikuwa, ingawa hakuwa na habari.

''Kulikuwa na giza hivyo hangeweza kuona mahali tulikuwa tumekaa. Sinema ilianza na video ya kwanza ilikuwa kutoka kwa baba yake, ilifuatwa na zingine kutoka kwa rafiki zake. Hapo ndipo nilitembea kuelekea alipokuwa,'' Bien alisema, akiongezea kuwa alimtungia mpenzi wake wa miaka nne wimbo wa mapenzi.

Siku moja baada ya kuposa, Bien kwa mara ya kwanza aliweka wazi maelezo ya jinsi walivyopatana.

''Siku moja nilipatana na msichana inje ya klabu hapo Museum Hill", aliweka kwenye mtandao wa Instagram.

Alikuwa anapitisha wakati na @emmanueljambo na wazo likanijia 'wee  ni mrembo kupindukia.' Mwezi uliofuata tulionana tena bila kukusudia katika sherehe na tukawa na maongezi. Nilipigwa na butwaa kwani sijawai patana na mtu msichana mrembo na mwenye akili kama yeye. Ana roho ya dhahabu. Ni ngao yangu wakati wowote, bega langu la lilia.''

 Bien atakuwa wa pili kwenye bendi ya Sauti Sol kufunga ndoa baada ya mcheza gita Polycarp Otieno kufanya harusi na mpenzi wake wa Burundi Bi Mandi mwaka jana.