Chiloba na Akombe wajibizana kuhusu mauaji ya Chris Msando

Chiloba
Chiloba
Aliyekuwa kamishna na tume ya uchaguzi IEBC Roselyn Akombe  amedia kwamba afisa  mkuu mtendaji za tume hiyo Ezra Chiloba amemtishia anyamaze kuhusiana na mauaji ya Chris Msando .

Akombe,  wiki jana  alikuwa  amefichua kwamba Msando ambaye alikuwa maneja wa ICT wa tume hiyo  alielekezwa ‘kichinjio’ na watu wlaiokuwa wakifanya kazi katika tume hiyo .

Alisema yuko tayari kutoa ushahidi endapo jopo la uchunguzi litaundwa kuchunguza mauaji ya Msando .

Siku ya juapili alitumia twitter kuchapisha parua pepe ambayo   amedai Chiloba alimtumia  akimtaka anyamaze kuhusu  hatuayake ya kutaka kufichua anayojua kuhusiana na mauaji ya Msando .

" Usiandike upya historia .unyamavu wetu sio leseni kwako’ ilisema barua pepe hiyo  iliyoandikwa na Chiloba

Akombe amesema vitisho vya Chiloba  ni dhihirisho kwamba mauaji ya Msando yalikuwa kazi ya ‘wandani’ katika tume ya IEBC

" Inathibitisha kwamba panahitajika kuwa na jopo la uchunguzi .Wakenya wanastahili kuambiwa ukweli’ Amesema  Akombe .

Hata hivyo Chiloba  ambaye anafanya ukulima  baada ya kuondoka IEBC mwaka wa 2018  hakuthibitisha kutuma au kukana kuituma barua pepe hiyo .

 “Really? No comment,” Chiloba  alisema kupitia ujumbe mfupi kwa gazeti la The Star alipoulizwa kuhusu parua pepe hiyo .

Akombe,  aliutangaza julai tarehe 30 kwamba yuko tayari kutoa ushahidi  mbele ya jopo la uchunguzi  endapo litaundwa kung’amua ukweli kuhusu mauaji ya ChriS Msado .