Chipukeezy atemwa na runinga ya Ebru. Mbona figisu figisu?

chipukeezy-tv-e1480576197555
chipukeezy-tv-e1480576197555
Mtalaam wa ucheshi nchini Chipukeezy ametokwa na povu na kuchapisha ujumbe kwa mashabiki wake katika mtandao wake maridhawa wa insta ulio na wafuasi milioni 1 kwa kile anachokitaja kuvurugika kwa mkataba wake na runinga ya Ebru. Licha ya kuwa mcheshi, staa huyu amekuwa kifua mbele kupigania nafasi na kuipa shavu sanaa ya wasanii chipukizi nchini.

Soma hapa:

https://www.instagram.com/p/B1nwGHeh1aO/

Mcheshi  huyu anahoji kuwa mkataba wake na runinga ya Ebru ulianza kutatizika wakati alianza kuwainua vijana kutoka vitongojiduni kutoka kisanaa. Vijana hawa ni kama Kartelo na Stivo Simple Boy ambaye  kwa sasa anatawala anga za burudani na ngoma hatari Mihadarati.

Soma hapa:

Chipukeezy anadai kuwa alitumiwa baruapepe na usimamizi wa kituo hicho akitakiwa kugoma kumshirikisha mcheshi mwenzake Kartelo. Kulingana na uongozi wa kituo hiki, Chipukeezy anatakiwa kuwa akiwahoji wakurugenzi na wageni wa haiba ya juu nchini wakiwemo wanasiasa.

Chipukeezy anasema kuwa hawezi kabisa kushawishiwa na mtu kuacha kazi ya kuwainua wasanii wachanga. Staa huyu sasa anasema kuwa kipindi chake kitaruka kupitia mtandao wake wa YouTube.

Mengine yanafuata...