chipukeezy-eric-omondi-e1511956399672-696x363

Chipukeezy avuruga mkataba akiwasaidia staa chipukizi. Ona anachotakiwa afanye

Baada ya fundi wa ucheshi nchini kuoenekana kukerwa na kile alichokitaja Ebru kubania ndoto yake na falsafa ya kuwatoa wasanii chipukizi, staa huyu ameamua sasa kuihamisha shoo yake katika mtandao wa You Tube. Uongozi unamtaka agome kabisa kumshirikisha Kartelo katika kipindi maarufu Chipukeezy Show kinachoruka kupitia runinga hio.

Mkataba kati ya Chipukeezy na Ebru umeingia shubiri baada ya baruapepe kutumwa ikimtaka atenge wakati mwingi akiwahoji wakurugenzi na wanasiasa maarufu nchini kama alivyoripoti staahuyu katika mtandao wake wa insta.

Soma hapa habari kemkem:

Chipukeezy atemwa na runinga ya Ebru. Mbona figisu figisu?

Chipukeezy sasa anasalia na maamuzi mawili. Kwanza, atii na afuate kanuni na amri za wakubwa wake au azidi kukaidi na kupoteza kazi yake ya utangazaji. Staa huyu anahoji kuwa atazidi kukiendesha kipindi hiki katika mtandao wa YouTube.

Mastaa wengi nchini wameonyesha kuipa nguvu nia ya kutoka kwenye kituo hicho huku Eric Omondi akionekana kuipa nguvu asilimia 100%. Kwa sasa Chipukeezy yupo nchini Tanzania na ameahidi kuwa atakaporudi ataanza kurekodi kipindi hiki na kuruka katika akaunti ya Chipukeezy TV kwenye YouTube.

Soma hapa upate uhondo:

Pasta Ng’ang’a mashakani kwa kutishia kudhoofisha nyeti za wanaume kanisani

Mcheshi huyu sasa anasema kuwa atakuwa anarekodi kila jumatatu sio hapa jiji la Nairobi tu bali ata kuzuru katika vyuo vikuu, shule za upili na vyuo vya kiufundi nchini katika mwamko wa kuinua talanta za wasanii changa.

 

 

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments