Christina Shusho asimulia ni kwa nini alitoka kwa ndoa yake

102920476_179357350198037_2896987603038032914_n (1)
102920476_179357350198037_2896987603038032914_n (1)
Mwanamuziki wa nyimbo za injili kutoka Tanzania Christina Shusho amesimulia kilichompelekea kutoka kwenye ndoa yake na mumewe mchungaji John Shusho.

Shusho amesema kuwa aliamua kuondoka kwa ndoa hiyo ili kuangazia namna ya kueneza Neno la Mungu.

Amesema kuwa alipokea mwito kutoka kwa Mola ambao ulimtaka kuondoka kwenye ndoa hiyo na kuendelea kumhudumia.

Mama huyo wa watoto watatu alisema walikaa pamoja na mumewe na kulizungumzia swala hilo na wakaafikiana.

“The truth is that this is an assignment and nothing more. God gave me this assignment during this season. It is therefore a must for me to leave and go fulfill that assignment,” Shusho .

Ameongezea kuwa Mumewe hakupuzilia mbali hatua ya kuondoka kwa kanisa lao walilokuwa wamejenga na kuamua kujenga lake mwenyewe.

Akiulizwa ni kwa nini hatumi picha yoyote ya mumewe kwa mitandao ya kijamii, Shusho alisema kuwa hiyo haitamfaidi kivyovyote vile.

“I do not post photos of my family because it does not bring in any money. If it does not earn me a thing then why should I post it?” Alisimulia Shusho.