Chuchuma ya Willy Paul kama tsunami. Octopizzo, Khaligraph Jones na Timmy waishobokea

69590548_1555730694600995_7286319883584541194_n_1___1568960809_96273
69590548_1555730694600995_7286319883584541194_n_1___1568960809_96273
Mastaa wakubwa wa muziki nchini wameonyesha mapenzi makubwa kwa mkwaju wa Chuchuma wa staa wa muziki Willy Paul.

Nyimbo hii inaonekana kupigiwa upatu mkubwa na mastaa wa muziki nchini akiwemo Octopizzo na Khaligraph Jones.

Sio kawaida kuona mastaa wakubwa wa muziki nchini wakiimba ngoma ya msanii mwenzao.

Hivi inaashiria kuwa ngoma ya Willy Paul ni moto mkubwa katika tasnia ya muziki nchini.

https://www.instagram.com/p/B2mi9shnDL-/

Soma hadithi nyingine:

Ngoma hii ilikuwa ifanyike kati ya staa wa Bongo Rayvanny na Willy Paul ila stima za ushikaji zikakata na Pozze akaamua kuifanya peke yake.

Aidha, Willy Paul juzi kati alikuwa anateta kuwa Rayvanny ameiba ngoma hiyo na kuchombeza baadhi ya mistari katika vesi ya ngoma ya Pepeta.

Pepeta ni mkwaju unaofanya vizuri katika mtandao wa YouTube huku kwa sasa ukipiga views Milioni 10.

Soma hadithi nyingine:

Rayavany alimshirikisha staa wa kihindi Nora Fatehi na kutoa bonge la Pepeta.

Ngoma ya Willy Paul Chuchuma haijafikia kutazamwa kwa wingi sana kama Pepeta.

https://www.instagram.com/p/B2mTjkgHxdZ/

Kando na hivyo ngoma hii inatamba kwa kasi na mastaa nchini wakiwemo Eric Omondi wamekunwa na mabiti hatari ya ngoma hii.

Katika mtandao wa insta, Eric, Octopizzo na Khalighraph Jones wanaonekana kuipatia ngoma hii nafasi kubwa.

Staa wa muziki Timmy T Dat hajaachwa nyuma katika kuipa nguvu ngoma hii.

https://www.instagram.com/p/B2jP2DrnH-R/