Chuo kikuu cha JKUAT chafungwa kufuatia mgomo wa wanafunzi

Police with teargas
Police with teargas
Chuo Kikuu cha JKUAT kimetangaza kufunga bewa kuu la chuo hicho baada ya vurugu na ghasia kushuhudiwa.

Kupitia taarifa iliyochapishwa chuoni Jumatatu, iliwaamrisha wanafunzi wote kutoka katika maeneo ya chuoni ifikapo saa 12 mchana.

"Wanafunzi wote wanaamrishwa kutoka bewa kuu chuoni ifikapo mwendo wa 12 mchana mara moja,"  Memo kutoka naibu wa chansela Robert Kinyua ilisema.

Kupitia memo, Kinyua amesema kwamba kamati ya seneti ilifanya mkutano wa dharura na kuafikia uamuzi huo.

Wanafunzi wa bewa la Juja wamekuwa wakiandamana kulalamikia utovu wa usalama chuo huku wakilaumu usimamizi wa chuo kwa kupuuza malalamishi yao.

Polisi walikuwa na wakati mgumu kukimbizana na wanafunzi waliowalaumu kwa kukosa kuimarisha hali ya usalama.

"Ukiwa kwa highway unanyangwaywa kila kitu. Comrades tibim!" baadhi yao walisikika wakisema.