Chuo kikuu cha Nairobi kimefutilia mbali mipango ya kurejelea shughuli zake septemba baada ya wafanyikazi wake watatu kupatikana na virusi vya corona .
Uamuzi huo umeafikiwa na senate ya chuo hicho baada ya kufanya mkutano siku ya jumatano .Naibu mhadhiri huu wa chuo hicho Stephen Kiama amesema senate sasa itatoa tarehe mpya za kufunguliwa taasisi hiyo . Mojawapo ya kinachoweza kuamuliwa ni kufunguliwa kwa chuo hicho katikati ya mwezi novemba endapo visa vya coronavirus nchini vitapungua .
Hata hivyo Kiama amesema mafunzo na masomo yataendelea kupitia nia za mitandao na hakuna mwanafunzi anayefaa kuhitimu mwaka huu atakosa kufanya hivyo . Waziri wa elimu George Magoha mwezi juni alikuwa ametangaza kwamba shule zitafunguliwa januari mwakani .hata hivyo kufunguliwa kwa taasisi za elimu ya juu kulitarajia kutegemwa kupungua kwa visa vya ugonjwa huo nchini .