Cliff Ombeta akosa tena kufika mahakamani katika kesi ya mauaji ya Willie Kimani

ombeta
ombeta
NA ABDI RIZACK

Wakili Cliff Ombeta alikosa tena kuhudhuria kikao cha kusikiza kesi ya mauaji ya marehemu wakili Willie Kimani iliyokuwa imepangiwa kusikizwa na jaji Jessie Lesit Jumatano.

Katika kesi hio, maafisa wa polisi wa Utawala Fredrick Leliman, Stephen Cheburet, Sylvia Wanjiku, Leonard Mwangi pamoja na afisa wa upelelezi Peter Ngugi walikanusha Mashtaka dhidi yao kuhusiana na mauaji ya Willie Kimani.

Kupitia msemaji wake siku ya Jumatano, Ombeta aliambia mahakama kuwa bado hajahisi nafuu na kwamba alikuwa anaendelea kupokea matibabu.

Tarehe Kumi na tatu mwezi huu kesi hio iliahirishwa baada ya mahakama kuarifiwa kuwa Ombeta alikuwa anaugua.

Jaji Lessit alimuagiza Ombeta kumkabidhi wakili mwingine majukumu yake kuakilisha washukiwa iwapo hatakuwa amepata nafuu kufikia tarehe 8 mwezi Agosti.

Wiki Iliopita wakili wa mshukiwa mmoja Peter Ngugi aliwapigwa kalamu hadharani mteja wake kuitisha wakili mwanaume badala ya mwanamke kumwakilisha.

Kesi hio inatarajiwa kusikizwa tena tarehe nane mwezi ujao.