Club 1824 kufungwa baada ya kuvunja sheria za virusi vya corona

Usimamizi wa club 1824 wakizungumza walisema kuwa wamefunga klabu hiyo ili kiweze kufanyiwa ukarabati, kwa muda sasa kimekuwa kikiwaruhusu raia kujivinjari na kuvunja sheria zilizotolewa na wizara ya afya ili kuthibiti virusi vya corona.

Ni klabu ambacho kinafahamika sana katika eneo la Lang'ata, siku chache baadae kilikashifiwa kwa kuvunja sheria hizo,

Kupitia mitandao ya kijamii, wasimamizi wa klabu hicho wamesema wamechukua hatua hiyo ili waweze kufanya ukarabati wa hapa na pale.

Hata hivyo, hawakusema ni kwa siku ngapi klabu hicho kitafanyiwa ukarabati au ni lini kitakapofunguliwa tena.

Klabu hicho kimekuwa kikimulikwa hivi karibuni kwa kuwaruhusu raia kuburudika licha ya serikali kupiga marufuku watu kukaribiana na mikusanyiko mikubwa.

Video iliyosambaa mitandaoni ikiwaonyesha baadhi ya raia wakiburudika katika eneo hilo iliwaghadhabisha wengi na baadhi kutaka mmiliki wake kuchukuliwa hatua za kisheria.

https://twitter.com/NationalERKe/status/1268030913495076867

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alilaani kitendo hicho na kuwarai Wakenya waendelee na kuchukua tahadhari za kudhibiti maambukizi zaidi ya virusi vya COVID-19.

Awali Lang'ata imekuwa ikisajili visa vipya vya virusi ya corona kila kuchao, ina maana kuwa wananchi wengi hawajafahamu kuwa virusi hivi vinasambaa kwa kasi?