CNN yaorodhesha Diamond Platnumz kama staa mkubwa Afrika, ona mchango wake

Screenshot_from_2019_11_26_15_57_09__1574773095_95673
Screenshot_from_2019_11_26_15_57_09__1574773095_95673
Kituo cha habari cha CNN kimeorodhesha Diamond Platnumz kama staa mkubwa Afrika.

Diamond amekuwa katika mstari wa kwanza kuupeleka muziki wa Afrika katika levo za kimataifa.

Kando na kuwa msanii, Simba ana mchango mkubwa sana katika jamii.

Lebo ya WCB imeweza kuwasimamia wasanii wengi na kuwafanya mastaa wakubwa Afrika Mashariki.

Wasanii hawa ni Rayvanny, Mbosso, Dadake Queen Darleen, Lava Lava.

Rich Mavoko na Harmonize walikuwa mastaa katika lebo hii na baadae kuitema na kushughulika na muziki wao.

https://www.instagram.com/p/B5TMxHcJVDD/

Aidha, Mondi ana mchango mkubwa katika kuwasaidia watoto walio na matatizo ya moyo.

Staa huyu alitangaza kuwa mapato ya fiesta ya Wasafi yangeenda kuwasaidia watoto hao.

Kando na moyo wa kufanya vizuri,Mondi anamiliki Wasafi TV na Wasafi FM.

Hii inampa nafasi nzuri ya kuweka katika nafasi za kwanza na shirika la kimaifa la CNN kama staa mkubwa Afrika.

https://www.instagram.com/p/B5R7Mm-hAlI/

Itazame orodha hapa:

1. Burna Boy – Nigeria

2. Angelique Kidjo – Benin

3. Diamond Platnumz – Tanzania

4. Yemi Alade – Nigeria

5. Tiwa Savage – Nigeria

6. Wizkid – Nigeria

7. Mr. Eazi – Nigeria

8. Sho Madjozi – South Africa

9. Busiswa Gqulu – South Africa

10. Mwila Musonda, aka Slapdee – Zambia