Collymore hadi Binyavanga: Watu mashuhuri walioaga dunia 2019

Ingawa taarifa hii inaangazia zaidi vifo vya watu maarufu wa Afrika mashariki walifariki mwaka 2019, tunaanza na kiongozi wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye kifo chake kiliitikisa dunia :

Pigo la kwanza lilikua ni Kifo cha aliyekuwa rais wa zaman wa Zimbabwe Robert Mugabe kilichotokea tarehe 6 Juni, 2019.

Mugabe aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 alikuwa nchini Singapore akipokea matibabu kwa muda mrefu.

2. Bob Collymore:

Haki miliki ya pichaCITIZEN TV
Image captionCollymore alianza kuuiongoza kampuni ya afaricom mwaka 2010
Kifo cha Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni kubwa zaidi ya mawasialiano ya simu Afrika Mashariki Safaricom, Bob Collymore kililitikisa eneo zima la Afrika Mashariki , huhusa ni kutokana na kifo hicho kutokea ghafla. Taarifa ya kifo chake ilitolewa na kampuni hiyo iliyosema kuwa aliaga dunia Juni Mosi 2019.

Kabla ya kifo chake Collymore, alichukua likizo ya matibabu ya miezi tisa mwishoni mwa mwaka 2017 na kuelekea nchini Uingereza kwa ajili ya matibabu ya saratani .Alirejea Kenya mwezi Juni mwaka jana.

Collymore alianza kuuiongoza kampuni ya Safaricom mwaka 2010.

Mwaka 2017 wanahisa walipiga kura kuongeza mkataba wa Bob Collymore kwa miaka miwili baada ya mkataba wake kuisha.

Mkataba aliokuwa akiufanyia kazi ulikuwa unatarajiwa kukamilika mwaka 2020 na kumfanya kuwa Mkurugenzi aliyekalia kiti hicho kwa muda mrefu zaidi kwenye historia ya kampuni hiyo.

Viongozi kadhaa wakiwemo Rais Uhuru Kenyatta walituma risala za rambirambi kwa familia kufuatia kifo hicho.

3. Binyavanga Wainaina:
Haki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionBinyavanga Wainaina, alikuwa miongoni mwa Wakenya wa kwanza kujitokeza hadharani na kusema kuwa yeye hushiriki mapenzi ya jinsia moja
Kifo cha Mwanaharakati wa haki za wapenzi wa jinsia moja, kilikua ni kifo kilichozungumziwa sana Kenya Afrika mashariki, na hata nje ya mipaka ya Afrika hususan kutokana na hali yake ya kijinsia.

Mwanaharakati huyo alifariki mwezi Mei akiwa na umri wa miaka 48, baada ya kuugua.

Wainaina alikuwa mshindi wa tuzo ya Caine na aliorodheshwa na gazeti la Times magazine miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani 2014.

Binyavanga Wainaina, alikuwa miongoni mwa Wakenya wa kwanza kujitokeza hadharani na kusema kuwa yeye hushiriki mapenzi ya jinsia moja.

4. Ruge Mtahaba:

Haki miliki ya pichaCLOUDS MEDIA GROUP TANZANIA
Image captionRuge Mutahaba amefariki Afrika kusini alikokuwa akipokea matibabu
Watanzania pamoja na tasnia ya habari kwa ujumla hususan katika eneo la Afrika Mashariki haitasahau tarehe 26 Februari, mwaka 2019 siku ambayo Luge Mutahaba alifariki dunia nchini Afrika Kusini alikokua akipata matibabu.

Mutahaba alizaliwa Mwaka 1970 nchini Marekani.

Muasisi mwenza na Mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga alielezea namna ambavyo Ruge atakumbukwa:

'Ruge ametutoka akiwa bado kijana mdogo kabisa, amefanya mambo mengi sana. Amepigana ameugua, amekuwa South Africa kwa muda tukipigania sana kuhakikisha anarudi katika hali yake ya kawaida, afya bora. 'Lakini Mungu amempenda na amemchukua siku ya leo, amueke mahali pema peponi'.

5. Ali Mufuruki:

Haki miliki ya pichaNMG
Image captionAli Mufuruki aliaga dunia nchini Afrika Kusini alipokuwa akipata matibabu.
Kifo cha hivi karibuni kilikuwa ni cha Ali Mufuruki, mfanyabiashara, muhisani na kocha wa masuala ya uongozi, ambaye alifariki dunia siku ya Jumamosi tarehe 07 mwezi huu wa Desemba akiwa na umri wa miaka 61.

Watu mbali mbali nchini Tanzania na nje ya taifa hilo watuma rambirambi zao hususan kupitia mitandao ya kijamii kufuatia kifo cha Bwana Mufuruki.

Mwenyekiti wa jukwaa la CEO Roundtable la Tanzania Sanjay Rughani alinukuliwa akisema Mufuruki alifariki katika hospitali ya Morningside ya jijini Johannesburg Afrika Kusini ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Mtendaji Mkuu wa jukwaa la sekta binafsi nchini, Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), Godfrey Simbeye alikitaja kifo cha Bwana Mufuruki kuwa ni pigo na pengo kubwa katika dira ya sekta binafsi nchini Tanzania.

Mufuruki alikuwa kiongozi aliyejali sana sekta binafsi nchini. Kila mara alikuwa tayari kutoa ushauri wake juu ya namna ya kuimarisha sekta hii. Tutazikosa sana busara zake.' Alisema Simbeye.

-BBC