Congratulations: Mama kutoka Kakamega kujifungua mapacha watano

Mwanamke wa miaka 28 aliweza kuvunja rekodi katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya Kakamega kwa kujifungua mapacha watano, hiyo ndio namba ya juu zaidi kwa hospitali hiyo mwanamke kujifungua mapacha watano.

Everlyne Namukhula kutoka kijiji cha Sisokhe eneo la Navakholo aliweza kujifungua wasichana watatu na wavulana wawili kupitia operesheni ambayo ilichukua muda wa masaa mawili.

Namukhula ana watoto wanne mapacha wakiwa ndani yao, mwanamke huyo ambaye alikuwa na furaha alisema kuwa watazungumza na mume wake waone kama wataweza kupata watoto wengine.

"Na mshukuru Mungu kwa kunipa watoto watano sasa wamekuwa tisa, nina amini kuwa usaidizi wa Mungu tutaweza kuwalea,

"Kwa maoni yangu nafikiria watoto hao wametosha, lakini nitajadiliana na baba yao tuone kama tutaweza kuongeza wengine." Alisema Everlyne.

Aliweza kuomba serikali imsaidie kuwalea watoto hao kwa maana sijambo la urahisi.

Mume wake ni mfanya vibarua ambaye anafanya kazi hiyo ili kuilinda na kuilisha familia yake, licha ya kuwa mfanya vibarua pia ana matatizo ya kusikia (kiziwi).

Namukhula aliweza kutoka katika hospitali ya kata ndogo Kakamega, Navakholo baada ya madaktari wa hospitali hiyo kujua amebeba zaidi ya mapacha na kisha kumuambia aende katika hospitali Kakamega.

"Mama na watoto watano, ambao kwa sasa wako katika chumba cha watoto, wako katika hali sawa pia tunamshukuru Mungu kwa ajili yake,

"Ambacho anahitaji kwa sasa ni chakula kizuri na pia dawa za kutosha ili aweze kupona." Alisema Dkt Githinji Ndung'u.

Ndung'u alisema kuwa aliweza kumpokea na kumfanyia matibabu kadhaa, aliongeza na kusema kuwa hiyo ndio namba ya juu ambayo wamama wameweza kujifungua katika hospitali hiyo, huku wengi wakiwa wanajifungua mapacha wawili au watatu.

Mkuu wa afya Racheal Okumu alimtembelea Namukhula na watoto wake nakusema kuwa Namukhula ataweza kupata usaidizi kupitia usaidizi wa Oparanya.

Ni programu ambayo imeanzishwa na Wycliffe Oparaya alisema pia mama huyo ataweza kusajiliwa kwa kadi ya NHIF na serikali ya kaunti kumlipia deni.

"Kama serikali ya kaunti tutafuatilia kwa sana mama na watoto wake na kuhakikisha kuwa yuko katika afya njema, na pia yeye na watoto wake wamekula kwa maana ndio viongozi wetu wa kesho." Rachael Aliongea.

Ni kisa ambacho kiliweza kuwavutia wananchi huku wakimpongeza mama huyo katika mtandao wa kijamii.