CORD Bado Hatujakubaliana Nani Atapeperusha Bendera Ya Urais - Kalonzo

rsz_kal
rsz_kal
Mheshimwa Kalonzo Musyoka asubuhi ya leo alikanusha madai ya seneta wa Machakos, Johnson Muthama kwamba muungano wa CORD tayari umeamua nani haswa atakayepeperusha bendera ya urais mwaka ujao.

Takriban wiki moja iliyopita, Seneta Muthama alidokeza hayo alipokuwa akihojiwa ndani ya studio ya Radio Jambo.

Nataka kuwaambia wananchi kuwa tunashindana na serikali ambayo ina pingu, pesa na vyombo vya uongozi. Ikiwa miezi hii kumi na moja iliyobaki tutaweza kumtoa kiongozi au kinara wetu, Jubilee watamtoboa tumbo hata kabla hajatoka ndani ya nyumba.” Alisema Muthama.

Kwa hivyo wasubiri tu, dereva tunamjua tushampa funguo tunamtafutia njia vile atapenya.

Kwa hivyo Jubilee wameweka mitego barabarani wanamngojea atokee, atobolewe macho, atobolewe masikio utumbo uteremke chini. Aliongeza akisema kuwa hawezi taja mgombea wao lakini “Siwei mtaja hata ukinipeleka Kamiti, wacha Pangani hata unipe dawa ya kuota.”

Lakini Kalonzo ambaye ni kinara wa chama cha Wiper alikanusha hayo huku akidai kuwa hayo ni maoni tu ya bwana Muthama na kuwa bado hawajaeleana wala kukubaliana nani atakaye beba bendera ya CORD.

"Hayo nadhani ni fikira za Muthama, kama anajua bado hajanieleza." Alisema bwana Kalonzo. "Wanaojuana ni sisi watatu, bado hatujaelewana. lazima tuweke wazi, hatujakubaliana ni nani atabeba bendera." Aliongeza Mheshimiwa ambaye aliwaitumikia nchi hii kama naibu wa rais katika kipindi cha 2008-2013.

Skiza kanda ifuatayo huku Kalonzo akizungumzia swala la wabunge na magavana waliohamia Jubilee na pia mbona muungano wa CORD hautavunjika hivi karibuni.

&feature=youtu.be