pjimage (17) (1)

Corona haitaki makasiriko nani! Tazama jinsi wanasiasa wa Kenya walivyojiweka karantini

NA NICKSON TOSI

Taifa la Kenya linafahamika sana kuwa na wanasiasa wanaoenzi siasa kila mara hata kama miaka ya uchaguzi mkuu haijafikia.

Baada ya virusi vya Corona kutua katika taifa la Kenya na Ulimwengu kwa ujamla, yamkini wanasiasa hawa wameonekana kama simba waalionyeshewa bila jukwaa za kupiga domo na kutulia majumbani mwao bila hata kuonekana kwenye vyombo vya habari kwa muda.

Hapa nimekuandalia tu baadhi ya wanasiasa hao, tazama.

Raila ,Kalonzo ,Uhuru,Mudavadi na Ruto.

Tangu serikali kuripoti visa vya Corona kuwasili nchini yapata juma moja unusu hivi lilopita, vyongozi hawa wamenyamaa zaidi na kuonekana kwa umma tu wakati wa maombi ya kitaifa katika ikulu ya rais.

Siasa zilizokuwa zimekita mizizi za no one can stop reggea sasa zimenyaaa,hazipo tena.

kalonzo

Kimani Ichungwa

Mbunge huyu anaegemea mrengo wa Tanga tanga unaompigia debe naibu wa rais William Ruto, hivi maajuzi ameonekana mtulivu baada ya kupiga picha akiwa kwa nyumba.

ichungwa

Bonny Khalwale

Corona imefanya mashindano ya ng’ombe almaarufu kama bullfighting kusitishwa hali iliyomfanya seneta huyu wa zamani wa Kaunti ya Kakamega kutulia nyumbani na familia yake.

Bullfighting ni baadhi ya tamaduni maarufu zaidi katika jamii ya Waluhya, magharibi mwa kenya.

bonny khalwale

Moses Kuria

Mbunge huyu wa Gatundu kusini tangu mkurupuko wa Corona kujiri nchini, amekuwa mchungaji wa kimitandao akieneza jumbe za kutaka wakenya kujiepusha na virusi hivyo.

moses kuria

Francis Atwoli

Katibu mkuu wa chama cha kutetea maslahi ya wafanyakazi nchini COTU, amekuwa akibarizi katika boma lake lililoko kaungti ya Kajiado na hajakuwa akionekana katika hafla mbali mbali nchini kwa hofu ya Corona. Katika video moja iliokuwa ikizunguka mitatandaoni anaonekana akiburushwa nyumbani kwake na mwanamziki akimporomoshea vibao vya rhumba.

atwoli

Junet Muhamed

Kwa wengine  kama Junet walipata fursa ya kutembelea miradi yao kabla ya maendeleo  katika eneo bunge lake.

junet (1)

Maisha yakiwa hivi nchini, bila shaka  tutaweza kupiga hatua kubwaa kimaendeleo bila siasa za kila mara.

 

Mhariri: Davis Ojiambo

Photo Credits: Radio Jambo

Read More:

Comments

comments