Corona ni wewe! Oparanya na Wamalwa kukutana na viongozi mjini Kakamega hii leo

Gavana wa Kakamega Wyclife Oparanya na waziri wa ugatuzi nchini Eugene Wamalwa wanatazamiwa kuandaa mkutano na viongozi kutoka eneo hilo hii leo.

Mkutano huo unatazamiwa kuangazia umoja wa jamii ya Mulembe haswa wakati huu ambapo mirengo tofauti ya kisiasa imeanza kushuhudiwa nchini.

Hivi maajuzi waliandaa mkutano sawia katika kaunti za Bungoma,Trans Nzoia, Busia na Vihiga.

Viongozi hao wamekuwa wakikutana tangu walipoidhinishwa kama wakuu wa jamii ya luhya na Francis Atwoli Mei 30, Kajiado.

Mkuu wa Michezo kaunti ya Kakamega Robert Makhanu ambaye pia ni katibu mtendaji amesema mkutano huo utafanyikia katika chuo kikuu cha Masinde Muliro.

“The meeting will be used by the leaders to communicate the government’s development agenda for the region. You know that they were appointed to spearhead the President’s development agenda in Western,” Makhanu

Mkutano huo unajiri wiki moja tu baada ya polisi kuwatanya wabunge waliokuwa wameitisha mkutano katika boma la Wetangula kutimuliwa.