Corona Robot: Tunisia yatumia roboti kuwazuia watu kutoka nje.

Robot
Robot
Wizara ya usalama wa ndani  ya  Tunisia  imeanza kutumia roboti  za polisi  ili kuwazuia watu kutoka nje  baada ya serikali ya taifa hilo kutangaza marufuku ya kutotoka nje ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona .

Roboti hiyo kwa jina  PGuard,  inaendeshwa  na maafisa walio katika sehemu ya mbali na inaweza kumtambua mtu aliye sehemu ya mbali kando na kuwa na kamera kadhaa.

Picha na sauti zinazochukuliwa na roboti hiyo zinawekwa katika  tovuti ya wizara ya usalama wa ndani  huku wanaokiuka agizo la kutotoka nje  wakiulizwa  maswali na roboti hiyo na kutakiwa kuonyesha vitambulisho  vyao.

Tunisia imekuwa chini ya marufuku ya kutotoka nje tangia Machi tarehe 17  na mamlaka ziliweka  masharti  makali kuzuia usafiri wa watu kuanzia tarehe 22 machi .

Nchi hiyo  imethibitisha visa  455 vya ugonjwa huo  huku watu 14 wakiaga dunia. Raia wa Tunisia  Anis Sahbani aliyetengeza roboti hiyo amesema iliundwa mwaka wa 2015 ili kufanya doria muhimu za usalama