oparanya

Corona yatua Magharibi mwa Kenya!Mwanafunzi wa miaka 19 apatikana na virusi vya Corona Kakamega

NA NICKSON TOSI

Gavana wa kaunti  ya Kakamega  Wycliffe Oparanya amethibitisha kuwa mwanafunzi wa miaka 19 mvulana aliyerejea nchini kutoka Uingereza amelazwa katika hospitali kuu ya kaunti hiyo baada ya kupatikana na virusi vya Corona.

Oparanya ameongeza kuwa mhudumu wa boda boda aliyembeba mwanafunzi huyo alipokuwa ametoka ughaibuni amepatikana na kwa sasa amewekwa chini ya karantini ili kubaini iwapo aliambukizwa virusi hivyo.

Familia ya mwathiriwa vile vile imewekwa chini ya karantini kufuatia tukio hilo.

19-year-old student in Kakamega tests positive for coronavirus, MCA quarantined

Gavana huyo pia amesema mwakilishi wa wadi ni miongoni mwa watu wanne walioshauriwa kujitenga na watu wengine baada ya kudaiwa kuwa walijumuika na mwanafunzi huyo.

 

 

 

Photo Credits: Radio Jambo

Read More:

Comments

comments