Corona yawanyima raha wafuasi wa Bongo Eldoret

NA NICKSON TOSI

Msanii Rayvanny kutoka taifa jirani la Tanzania amelazimika kufutilia mbali tamasha lake la mziki lililokuwa linatarajiwa kuandaliwa Eldoret Sports Club mnamo Aprili 11 mwaka huu kutokana na Corona.

Katika ujumbe wake kwa mashabiki wake ,Rayvanny aliwadokeza kuwa kutokana na hofu ya kuenea kwa virusi hivyo,waandalizi wa tamasha hilo watatoa tarehe mwafaka ya kufanyika.

"Watu wangu wapendwa wa  254🇰🇪🇰🇪🇰🇪 tamasha letu limefutiliwa mbali kutokana na hofu ya virusi vya Corona 😭 !! tusubiri tangazo lingine ambalo tutatoa tarehe mwafaka ... 🙏🙏" aliandika Rayvanny.

Siku chache zilizopita,Diamond alilazimika kufutilia mbali tamasha lake ughaibuni wakati ambapo alikuwa alikuwa anatarajiwa kuwatumbuiza mamia ya mashabiki wake ,lakini kutokana na amri za baadhi ya mataifa ya kutaka wananchi wake waepukane na maeneo yaliyojaa watu,ilipelekea tamasha hilo kusongeshwa .