'Coronavirus inaweza kutibiwa ': Mgonjwa wa kwanza wa Kenya Brenda azungumza

Ugonjwa huu unaweza kutibiwa, mgonjwa wa kwanza wa coronavirus nchini, Brenda Cherotich  amesema.

Mwanadada huyo aliyetambuliwa kama Brenda  alizungumza  wakati yeye na mgonjwa mwingine kwa jina  Brian walipozungumza na rais Uhuru Kenyatta kupitia njia ya Video.  Wagonjwa hao wawili waliopona walikuwa wameandamana na waziri wa afya Mutahi  Kagwe katika jumba la  Afya. Brenda aliwahimiza wakenya  kuwajibika na  kuripoti kwa maamlaka pindi wanapopata daalili za virusi vya Corona .

" Wasiliana na maamlaka na ujitokeze  mnapema, nilisafiri kwenda Marekani mwezi Disemba na kuchukua ndege nyingine hadi London, nashuku ni wakati huo nilipopata virusi hivyo’ amesema .

Brenda  amesema akiwa Marekani alifahamu kwamba kulikuwa na kituo cha kuwatenga wagonjwa katika hospitali ya Mbagathi .

‘ Nilipowasili Kenya  nilikuwa na kikohozi kwa siku tatu, niliendelea kutathmini hali yangu na baadaye nikaamua kwenda hospitali ya Mbagathi siku ifuatayo’ amesema Brenda .

" Madaktari walichukulia kisa changu kwa uzito uliostahili  na wakanipa  barakoa. Nimekuwa katika karantini kwa siku 23, na nilitunzwa vyema’.

Anasema wauguzi wakati mwingine walikuwa chini ya shinikizo na walikuwa wakimuita ‘mgonjwa wa kwanza’.

Alipokuja Kenya, alitangamana na rafiki  yake Brian .

" Nilipata virusi hivyo kutoka kwa Brenda . Pindi matokeo yake yaliporejea na kuonyesha kwamba alikuwa mgonjwa , nilijua pia mimi ninao. Naishukuru serikali kwa kuja kunichukua na kunipeleka kwa  kituo cha afya cha umm ambako nimetibiwa kwa wiki mbili’ Brian amesema

Wakati wa mazungumzo na  wawili hao, rais Uhuru aliwasifu Brenda na Brian kwa ukakamavu wao.

" Tufuatane mfano wa Brenda na Brian. Tunaweza kuthibiti virusi hivi. Kwa wote walio na dalili hizi waripoti mara moja kwa maamlaka husika, tujitambue mapema ili  tupewe matibabu …’ rais Uhuru amesema

Uhuru amesema pindi wawili hao watakapomaliziwa na madaktari, angependa kukutana nao ana kwa ana katika Ikulu. Kenya iliripoti kisa cha kwanza na virusi vya Corona Machi tarehe 13 . Taifa kwa sasa lina visa 59  vya walioathiriwa na coronavirus na kifo  cha mtu mmoja aliyeaga dunia kwa ajili ya virusi hivyo.