Michezo 2

Coronavirus :Mchuano wa Barcelona v Napoli kuchezwa bila mashabiki

Mchuano wa kombe la mabingwa kati ya barcelona na Napoli tarehe 18 mwezi huu utasakatwa katika uwanja uliofungwa waa Nou Camp kwa ajili ya hofu ya virusi vya Corona .

Mechi za kombe la mabingwa,awamu ya 16 bora

” Uamuzi huo umefanywa kwa minajali ya  sababu za kiafya’ amesema  afisa mkuu wa  afya  wa serikali ya jimbo la  Catalunya Joan Guix. Mchuano huo ni wa pili kati ya timu za  uhuspania na italia katika ligi ya mabingwa kusakatwa bila mashabiki baada ya mchuano wa Valencia dhidi ya Atalanta jumanne wiki iliyopita . Mchuano wa Getafe  na Inter Milan katika kombe la bara Uropa  pia uliishia hatma hiyo .

Mchuano wa kombe la mabingwa kati ya  Paris St-Germain  na  Borussia Dortmund  siku ya jumatano pia utakosa mashabiki . shughuli zote za michezo nchini Italia zimesitishwa  hadi Aprili tarehe 3 kwa ajili ya hofu ya virusi vya Corona . Agizo hilo litaathiri pia mechi za kombe la Serie A  lakini sio timu za italia au vilabu vinavyoshiriki mashindano ya kimataifa.

Shujaa:Tazama mchango wa Marehemu Tony Onyango katika raga ya kenya

Ripoti zaarifu kwamba La liga huenda ikatoa tangazo kwamba mechi zake zijazo zitasakatwa katika viwanja visivyokuwa na mashabiki . mchuano wa Manchester united wa kombe la bara uropa raundi ya 16 bora dhidi ya  LASK Linz  nchini Austria  siku ya alhamisi  huenda pia ukachezwa katika uwanja mtupu bila mashabiki

Photo Credits: Yusuf Juma

Read More:

Comments

comments