Coronavirus: Mgonjwa wa kwanza apona Kenya, huku marufuku ya kutoka nje ikitangazwa

huduma
huduma
Kenya imetanza kupona kwa mgonjwa wa kwanza aliyekuwa ameambukizwa virusi vya corona.

Rais Uhuru Kenyatta ametangza habari hizi njema alipokuwa akihutubia taifa. Rais Kenyatta  hata hivyo ametangaza visa vitatu zaidi vya maambukizi ya virusi vya Corona na kufikisha idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi hivyo nchini hadi 28.

Rais amesema kupona kwa mgonjwa huyo ni ishara kwamba ugonjwa huo unapona na kuhimiza wakenya kufuata masharti ya serikali.

Rais ameshtumu baadhi ya viongozi hasa wa kiasiasa na wa kidini kwa kupuuza maagizo ya serikali kuhusu kuzuia maambukizi ya virusi hivyo. Amesema inasikitisha kwamba baadhi ya viongozi wa kisiasa na wale wa kidini wameambukiza watu virusi hivyo kwa kukaidi maagizo ya serikali.

Kufuatia kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya virusi hivi serikali imetangaza hali ya kutotoka nje kuanzia siku ya Ijumaa Machi 27, kati ya saa kumi na moja jioni hadi saa  moja asubuhi. Ni maafisa wa huduma muhimu pekee watakaoruhusiwa kutembea wakati huu. Orodha ya wafanyikazi muhimu ni kama ifuatavyo;

Katika juhudi za kuwakinga wafanyikazi wenye umri wa juu na wale wenye matatizo ya kiafya rais ameagiza wafanyikazi wote wa serikali wenye zaidi ya umri wa miaka 50 na wenye matatizo ya kiafya kwenda likizoni.

Naibu gavana wa Kilifi Gideon Saburi amezua mjadala nchini baada ya kukaidi agizo la serikali kujitenga alipowasili nchini kutoka Ujerumani na kisha kupatikana na virusi hivyo siku chache baadaye huku akiwa tayari ametangamana na watu kadhaa.