Coronavirus: Uhispania ni ya pili sasa kwa vifo vilivyotokana na Corona duniani

Idadi ya vifo imeongezeka kwa watu 738 ndani ya saa 24 kila siku na kufanya idadi ya vifo hivyo mpaka sasa kufikia 3,434, idadi ambayo iko juu zaidi ya Italia.

Ukilinganisha taarifa rasmi za China ambazo ziliripoti vifo 3,285 huku nchi ambayo imeathirika zaidi duniani, Italia ikiwa na vifo 6,820.Idadi ya maambukizi Uhispania imeongezeka mara tano na karibu watu 27,000 wanatibiwa kila siku hospitalini.Pamoja na mazuio mengi duniani bado virusi vya corona vinaonekana kuwa changamoto kubwa duniani, mpaka sasa dunia ina wagonjwa 460,000 na vifo zaidi ya 20,000 huku watu zaidi ya 110,000 wamepona ugonjwa huo kwa mujibu takwimu za chuo kikuu cha Johns Hopkins .

Wakati huohuo Marekani ikiwa kwenye hali tete ambapo visa 70,000 vya virusi vya corona vimethibitishwa na vifo vyapatavyo 1,050 .Idadi ya maambukizi imeonekana kuongezeka kwa zaidi ya 10,000 kwa siku moja.Ingawa si habari mbaya tu imepatikana kwa Marekani, kwa sababu gavana wa New York amesema kuwa hatua za makatazo yaliyowekwa yameanza kutekelezwa kikamilifu na matokeo wameanza kuyaona.

Huku China katika jimbo la Hubei, ambako maambukizi ya virusi hivi vya corona vilianzia hali ikiwa shwari na hakuna maambukizi mapya yaliyoripotiwa.Hatahivyo idadi kubwa ya maambukizi yaliyotokea China yameripotiwa.Kwa upande wa Uingereza vifo vimeongezeka na kufikia 463 awali vilikuwa 422, wakati maambukizi ya ugonjwa huo yakiwa zaidi ya 9,500.Takwimu mpya za maambukizi ya virusi vya corona maeneo mbalimbali duniani

Kuna rekodi ya maambukizi 470,000 duniani kote..

Idadi ya vifo ni 21,270 huku waliopona wakiwa 114,000

  • China -Wagonjwa 81,667 , vifo 3,285 , Waliopona 73,775
  • Italia - Wagonjwa74,386,vifo 7,503 Waliopona 9,362
  • Marekani -Wagonjwa 70,000 , vifo, 1,031 Waliopona, 616
  • Uhispania- Wagonjwa 49,515 vifo 3,647 Waliopona 5,367
  • Ujerumani -Wagonjwa 37,323, vifo- 206 , Waliopona 3,547
  • Iran -Wagonjwa 27,017 , vifo, 2,077, Waliopona9,625
  • Ufaransa- 25,600 vifo, 1,333 , Waliopona3,907
  • Switzerland- 10,897 vifo 153 ,Waliopona 131
  • Uingereza 9,640 vifo 466 , Waliopona 140