Coronavirus : Walivuta matiti yangu na kusema, 'Wewe sio mwanamke '

Na BBC

Amri ya kutotoka nje nchini Panama inatekelezwa kwa utaratibu, ambao unawaruhusu wanaume kutoka nje siku moja na wanawake situ inayofuata. Lakini utaratibu huo umetumiwa kama kisingizio cha kuwanyanyasa mahuntha (watu walio na jinsia mbili) katika jamiii.

Monica ni mpishi hodari. Sawa na watu wengine, wakati huu wa lockdown amekuwa akiandaa chakula kama njia ya kujiliwaza kutokana na hali ya kukaa ndani kwa muda mrefu.

Jumatano moja mwezi uliyopita, Monica aliamua kupika kuku wa kupaka iliyochanganywa na viungo vingi na pamoja na Roba la tomato la kulia na wali.

Alikuwa karibu na viungo vyote, lakini alitaka kununua kuku. Kwa hivyo alitoka katika nyumba yake ndogo iliyopo karibu na uwanja wa ndege wa mji wa Panama ambayo anaishi pamoja na familia take na kwenda dukani.

Alikutana na kundi la wanawake akiwa njiani, baadhi yao wakiwa wamewashika mikono watoto wao. Ilikuwa jambo la kawaida katika mtaa huo, kwani serikali ilikuwa ndio mwanzo imebuni sheria mpya ya kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona, kwa kuwaruhusu wanawake kutoka majumbani mwao kununua bidhaa muhimu siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa.

Na wanaume wakiruhusiwa kutoka Jumanne , Alhamisi na Jumamosi. Siku ya jumpili kila mtu anatakiwa kusalia nyumbani.

Monica aliingia dukani. Alifahamu familia ya Wachina waliokuwa wakiendesha duka hilo vizuri. Walimpenda sana.

Lakini alipoingia katika duka hilo ,mazingira yalidalika. Mwenye duka alimfikia kwa upole, na bila tabasamu alilozoea kumuona nalo usoni kila alipofika dukani hapo na kumwambia.

"Hatuwezi kukuhudumia, Monica," alisema. "Polisi walitoa maagizo kuwa wanawake pekee ndio watakaohudumiwa leo. Walisema, 'hakuna maricon.'"

Neno linalotumiwa kuwatambulisha watu wenye jinsia mbili. Monica hakushangazwa kusikia maneno hayo kutoka kwa mwenye duka, kwani polisi patika mtaa huo walishawahi kumlenga kutokana na maumbile yake kama mwanamke huntha.

Baadae mwenye duka alimuelezea Monica kilichomfanya achukuwe hatua hiyo na kuomba msamaha huku akimwambia haikuwa mapenzi yake kumwambia aondoke dukani kwake. Ilikuwa maelekezo kutoka kwa polisi.

Monica alianza kuenda shale akivalia kama msichana akiwa na umbra wa miaka 12. Hakuwahi kujihisa kama mvulana, na sasa anataka kuangazia hali yake.

Kujitambulisha kama msichana hakukua na athari yoyote katika maisha yake ya kill siku nyumba - tayari alikuwa amepitia changamoto nyingi.

"Baba yang alikuwa mkali," Monica anasema. "Hakuhitaji sababu yoyote kunipiga mimi, dada zing wawili na mama yetu."

 

Monica pole pole alianza kubadili muonekano wake na kutengeza nywele zake kama mwanamke na hata kuvalia nguo za kubana. Shuleni alizomewa na wanafunzi wenzake kutokana na muonekano wake , jambo lililomfanya kujitenga na wenzake.

Lakini alifarijika kwa kupata upendo na urafiki aliopata kutoka kwa dada zake na uiendo wa mama yake.

Alipofikisha, umri wa miaka 14, baba yake akafariki ghafla na hapo ndipo maisha ya familia yake ikageuka kwa kwa kukosa mtegemezi.Monica alionelea ni bora asaidie familia yake kujikimu kimaisha.

Aliwahi kusikia kuwa wafanyikazi wa ngono walio na jinsia wanapendwa sana mjini Panama, na kwamba mapaoto ni mazuri.

Monica, akiwa mtoto mdogo aliamua, hiyo ndio njia pekee ya kusaidia familia yake.

Japo biashara ya ngono imehalalishwa Panama,hiyo haimaanishi hakuna ubaguzi, na Monica anasema polisi katika mji huo wamekuwa wakimyanyasa kwa miaka kadhaa.

Kwa mfano wamekuwa wakiendesha piki piki karibu yake na kutoa matamshi ya kibaguzi dhidi ya watu walio na jinsia mbili alipokuwa akienda kazini.

Akiwa na miaka 38 sasa, anasema amezoea kuishi kwa kubaguliwa kwa miaka 24.

"Watu wengi walio na jinsia mbili wamekuwa wakifanya biashara ya ngono katika mji huu," Monica anasema. "Je hii nadir njia pekee ya kujikimu kimaisha? La hasha, lakini ndio nji arahisi ya kusaidia familia yangu."

Tangu marufuku ya kutotoka nje ilipoanza kutekelezwa, hali imekuwa ngumu kwao baada ya biashara kusitishwa.

Alipofika kwa nyumba baada ya tulip la pale dukani, Monica alipokea jumble WhatsApp. Ulikuwa kutoka kwa mwenye duka. Alisema kuwa alijihisi vibaya kwa kukataa kumhudumia na kumuomba awatume dada make wakamchukulie kuku aliyetaka kununua, ama ampelekee yayeye mwenyewe.

MMonica alitabasamu. Kulikuwa na ukarimu katika jamii yake ambao utasaidia wkati wa lockdown. Lakini hakutaka kutegemea misaada kutoka kwa watu wakati wa janga hili la corona. Alitaka kuendelea na jukumu la kutunza familia yake.

Aliamua kutoka tena kwenda dukani siku iliyofuata ambayo ni siku iliyotengewa wanaume kutoka.

Lakini wakati huo hali ilikuwa mbaya zaidi kwake kutokana na jinsi alivyochukuliwa.

Aliamua kuenda katika duka kubwa la jumble kununua vita ambavyo kwa siku kadhaa.

Alipofika na kujiunga kwenye foleni ya kuingia dukani, aliingiwa na wasiwasi huenda akachelewa.

Chini ya sheria ya amri ya kutotoka nje nchini Panama watu waliruhusiwa kutoka angalau mara tutu kwa wiki laking kuna siku zingine waliruhusiwa kutumia muda wa saa mbili pekee nje kulingana na mahali out anapoishi.

Monica alisubiri kwenye foleni kwa ya wanaume, ambao hawakufurahia kumuona.

Muda ulikuwa unayoyoma na baada ya hapo sea miili zikawa zimeisha.

Karibu kila wakati, maafisa sita wa polisi walimfikia Monica, na kumtoa kwenye foleni yeye pekee yake.

"Waliniambia nilikuwa nje ya muda uliyowekewa wa kuenda dukani," anasema. "Walianza kunikagua mwilini. Mmoja wao alinifinya maziwa, na kwanza kucheka huku akisema, 'Wewe ni mwanamke,'huku akitumia maneno ya kudhalilisha watu walio na jinsia mbili."

Kila mimosa aliangalia kando na hakuna aliyejihusisha nae wala kujaribu kumsaidia. Monica hajawahi kujihisi mpweke hivyo.

Chama cha kutetea haki ya watu walio na jinsia mbili nchini Panama, kinasema visa vya watu hao kubaguliwa vimeongezeka, na kwamba zaidi ya watu 40 wamewasiliana nao wakilalamikia kunyanyaswa wanaoenda kununua bidhaa mbali mbali katika maduka ya jumla ama kuenda kununua dawa.

Mapema mwezi Mei, mamlaka nchini Colombia, katika mji mkuu wa Bogotá, iliammua kuondoa masharti yanayoegemea jinsia ya watu baada ya kuubaini kuwa mashariti kama hayo yanatumiwa kuwabagua wapenzi wa jinsia moja amma watu walio na jinsia mbili.

Baada ya Shirika la kutetea haki la Human Rights Watch, kuwasilisha waraka rasmi kwa rais wa Panama, kulalamikia hatua ya polisi kuwanyanyasa watu walio na uhuntha, wizara ya Panama inayosimamia usalama wa watu imetoa taarifa wiki hii kusema kuwa "imetoa maagizo kwa kikosi hicho kujiepusha na visa vyo vote via ubaguzi wa kijisia dhidi ya makundi maalum katika jamii" wakati wanapotekeleza amri ya kutotoka nje.

 

Monica hata hivyo Anatolia shaka agizo lililotolewa na wizara hiyo litamhakikishia usalama wake. Kwani alienda benki baada ya agizo kutolewa - siku ambayo ilikuwa zamu ya wanawake kuruhusiwa kutoka nje ya nyumba - na polisi mmoja alimfuata na kumwambia.

"Ningeenda nyumbani kama mimi ningelikuwa wewe," alimwambia. "Nasema hili kwa upendo, lakini hutakiwi kuwa nje leo."

BBC ilitaka Wizara ya usalama wa umma ya Panama kuangazia suala hilo, lakini haikutoa tamko lolote.

"Sijui nifanye nini. Nastahili kutoka lini nje?" Monica anauliza. "Sijaribu kumpumbaza mtu yeyote. Kile ninachotaka ni kusaidia familia yangu."