Mwanamme mwenye umri wa miaka 47 ametengwa katika wadi maalum huko Londiani katika kaunti ya kericho kwa kushukiwakauwa na virusi vya corona .
Mwamanamme huyo alipelekwa katika hospitali hiyo na mkewe baada ya kulalamikia maumivu ya viungo vya mwili na kukohoa ,daalili ambazo madaktari wanasema ni za virusi vya Corona .Ni mhubiri anayeripotiwa kuwasili kericho maajuzi kutoka mkutano huko Mombasa na kisa hicho kiliripotiwa sikau ya jumamosi lakini kikafichuliwakwa umma siku ya jumatatu .
Gavana wa Kericho Paul Chepkwony na afaisa mkuu anayesimamia huduma za matibabu David Ekuwam wamethibitisha kisa hicho.Mke wa mwanamme huyo ameshauriwa kusalia nyumbani ili kufahamu hali yake .