Coutinho kukataa ofa ya kujiunga na Manchester United

Kiungo wa Barcelona Philippe Coutinho mwenye umri wa miaka 27, atakataa ofa ya kujiunga na Manchester United, akiwa na malengo ya kuelekea klabu Paris St-Germain, japo anaweza pia kukubali kurejea Liverpool.

Liverpool pia wamejiunga kwenye kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili mshambuliaji wa CSKA Moscow Fedor Chalov mwenye thamani ya pauni milioni 20. Arsenal, Manchester City, Tottenham, Chelsea na Manchester United pia wanamnyemelea mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.

Manchester United hawatamuuza kiungo Mfaransa Paul Pogba kwenda Real Madrid iwapo miamba hao wa Uhispania watawasilisha ofa yao baada ya dirisha la usajili kufungwa kwa upande wa Uingereza, Agosti tarehe 8.

Manchester United imeafikiana na Leicester makubaliano ya thamani ya pauni milioni 80 kumsajili Harry Maguire na kumfanya kuwa mlinzi mwenye thamani kubwa katika historia. United italipa pauni milioni 60 kumsajili mchezaji huyo mwenye miaka 26 atakayefanyiwa ukaguzi wa kiafya leo na pauni milioni 20m za ziada katika siku zijazo.

Leicester nayo inatarajiwa kuijaza nafasi ya Maguire kwa kumsajili mchezaji wa Brighton Lewis Dunk, baada ya kuafikiana kwa mkataba wa pauni milioni 45 kwa mchezaji huyo wa miaka 27.

Celtic wamekataa ofa ya hivi punde ya Arsenal kumtaka mchezaji Kieran Tier-ney.

Ofa ya Arsenal offer ilikua ya thamni ya pauni milioni 25 lakini inaamikina kwamba Celtic hawakufurahishwa na mfumo wa ofa hiyo na wanataka pesa zaidi mara moja badala ya marupurupu.

Napoli pia wanamtaka Tierney, ambaye mkataba wake unakamilika mwaka 2023. Mchezaji huyo wa umri wa miaka 22 anaendelea kupona baada ya kufanyiwa upasuaji.