Mashabiki wa AFC Leopards wazidi kumwoboleza Felix Shitsama

68914602_10213714997941365_6975131114675372032_n
68914602_10213714997941365_6975131114675372032_n
Kakamega fraternity of AFC Leopards is mourning the death of former club vice chairman Felix Shitsama who perished in a road accident on Friday.

Wakaazi wa kakamega na mashabiki wa klabu ya AFC Leopards wanaendelea kumwomboleza aliyekuwa naibu rais wa klabu hio, Felix Shitsama aliyeiaga dunia siku ya Ijumaa baada ya kupata ajali ya barabara katika eneo la Timboroa. Felix alikuwa anaelekea mjini Malava  akiwa na maarafiki zake kwa ajili ya matanga ya mmoja wa wanafamilia wake.

 "Nipigo kubwa sana kwetu sisi kama klabu na familia ya AFC Leopards. Felix alikuwa kijana aliyejitolea sana na kila jambo alilohusika nalo. Shitsama atabaki kuwa kwenye viyabu vya kumbukumbu vya klabu ya  Leopards uaminifu wake kwetu sisi," mwenyekiti wa Leopards, Dan shikanda alisema.

Shitsama alichaguliwa na kama naibu wa rais wa klabu ya AFC Leopards mwaka wa 2016 chini ya uongozi wake Dan Mule. Shitsama anakubukwa kwa kufadhilisha dili baina ya klabu ya AFC Leopards na kampuni ya Umbro inayotengeza jezi zao kwa sasa.

"Wakati mwingine, Felix alikuwa anawatia motisha wachezaji akiwa peke yake pamoja na kuwaleta wachezaji wapya wanaoisaidia Leopards kwa sasa."

Juzi jumapili,Klabu ya AFC Leopards iliita mashabiki wote ili wamwelekezee Mola matatizo yao. Kulingana naye Dan Shikanda, klabu hio iliamua kumwomba mwenyezi mungu usaidizi ili iweze kujikomboa na majinamzi yanayo iadama kwa sasa.