COVID 19: Akina mama walio na corona wanaweza kuwanyonyesha wanao ili mradi wavalie maski-Wizara ya afya

Akina mama walio na  virusi vya Corona wanaweza kuwanyonyesha wanao  ili mradi wavalie maski ,wizara ya afya imesema

Wakati wa kikao na wanahabari  afisa mmoja mkuu katika wizara hiyo  Dr Pacifica Onyancha  amesema  akina mama wanafaa kuwaacha wanao kutunzwa na mtu mwingine pindi wanapomaliza kuwanyonyesha .

Pia  amewakumbusha wazazi  walo na watoto walip chini ya umri wa miaka miwili kutowavalisha maski kwani hatua hiyo inaweza kuhatarisha maisha ya wanao .

" watoto ni viumbe dhaifu sana … maski inaweza kuhatarisha maisha yao kwani inapunguza kiasi cha hewa wanayopumua’ Onyancha amesema

Onyancha pia amesema watoto walio chini ya umri wa miaka 5 hawafai kuvalia maski wakiwa ndani ya gari  kwani wanaweza kulala na kisha kukosa pumzi .Kenya  jumanne ilirekodi visa vipya 133 vya virusi vya corona na kufikisha jumla ya visa   3,860.

Visa hivyo vilipatikana baada ya sampuli  3,255  kupimwa katika saa 24 zilizotangulia .waziri wa Afya Mutahi Kagwe  amesema hadi kufikia sasa Kenya imepima sampuli  121,926.