Covid 19 : China yatumia Miti shamba kupambana na virusi vya corona

Miti shamba
Miti shamba
Huku watalaam  wakiendelea na juhudi za  kutengeneza chanjo ya virusi vya corona, China ambayo imekuwa mstari wa mbele  katika utengenezaji wa dawa za asili imetengeneza dawa ya asili inayojulikana kama 'Traditional Chinese medicine (TCM)' ili kutibu ugonjwa wa corona.

Gazeti moja lilizinduliwa na serikali ya China lilidai kuwa 92% ya wagonjwa wa corona wa nchi hiyo walitibiwa na dawa hiyo.

TCM ni dawa ya kale zaidi duniani ambayo imetengenezwa kwa mitishamba.

Dawa hiyo ni maarufu sana nchini China licha ya kwamba ilizua mjadala kuhusu matumizi yake mtandaoni.

Wataalamu wanasema China inajaribu kuisambaza dawa hiyo ya TCM ndani ya nchi na nje ya nchi lakini wataalamu wa afya bado hawaamini uwezo wake wa kutibu.

Wizara ya afya ya China imeweka kitengo maalum cha TCM pamoja na muongozo wa kukabiliana na virusi vya corona, wakati televisheni ya taifa ilidai kuwa dawa hiyo ilifanya kazi katika mlipuko wa maradhi miaka ya nyuma kama Sars mwaka 2003.

Kuna dawa sita ambazo zimekuwa zikitangazwa kutibu virusi vya corona, dawa mbili ambazo ni maarufu moja ni 'Lianhua Qingwen' - ambayo ni mchanganyiko wa dawa za mitishamba 13 kama vile forsythia na rhodiola rose - na Jinhua Qinggan - ambazo zilizinduliwa mwaka 2009 katika mplipuko wa H1N1 na ilitengenezwa na mchanganyiko wa vitu 12 vikiwemo asali, majani ya 'mint' na mizizi ya mmea wa 'liquorice'.

Wanaounga mkono dawa ya TCM wanadai kuwa hakuna madhara yoyote ukitumia dawa hizo lakini wanasayansi wanasema ni muhimu kwa vipimo vya kisayansi kufanyika ili kuhakikisha usalama wa dawa hiyo.

Taasisi ya afya Marekani ilisema labda dawa hiyo itasaidia kuondoa dalili lakini suala la kutibu corona bado kuna mashaka.

"Kwa upande wake hakuna ushaidi wowote mzuri ambao unaweza kudhibitisha matumizi yake hivyo kuna hatari ambayo bado haijaweza kuelezewa," Edzard Ernest, ni mtafiti wa zamani wa Uingereza wa dawa ambazo zimeunganishwa, alinukuliwa akisema hivi karibuni kuwa ni safari ya asili.

Aidha dawa ya TCM inazidi kupata umaarufu nchini China na inaonekana kuwa kuna hitajiko kubwa la kimataifa.

Baraza la taifa la China, mwaka jana lilikadiria kuwa kiwanda cha TCM kitakuwa na thamani ya dola bilioni 420 (£337bn) ifikapo mwishoni mwa mwaka 2020.

Rais Xi alisema kuna watu wengi ambao wanapenda dawa hiyo tangu enzi za mababu China na kuiita kuwa hazina ya watu wa China.

Lakini Yanzhong Huang, mtaalamu wa afya wa wizara ya mambo ya kigeni, amebainisha kuwa usalama na ufanyaji kazi kiufasaha ndio jambo linaloangaliwa katika dawa ya TCM na watu wengi wa China bado wanaona dawa za kisasa ni bora zaidi ya dawa za miti shamba kama TCM".

Taasisi ya kitaifa ya chakula na dawa nchini China ilibaini sumu katika sampuli ya TCM.

Licha ya kwamba China kuwa na juhudi ya kuisambaza TCM kimataifa , watu wengi nje ya China wamekuwa hawaifahamu.

Wakosoaji wanasema China kwa sasa inatumia mkurupuko wa virusi vya corona kuitangaza dawa hiyo nje ya nchi na kudai kuwa dawa hiyo imekataliwa katika vyombo vya habari vya taifa.

Hata hivyo China imekuwa ikisambaza dawa yake ya TCM pamoja na vifaa vyake katika mataifa ya Afrika, Asia na ulaya.

"Tuko radhi kushirikiana na wenzetu uzoefu wa China na suluhisho la China katika kutibu Covid-19, na kuruhusu mataifa mengine kufahamu na kuielewa dawa ya Kichina pamoja na kuitumia dawa hiyo ," Yu Yanhong, Naibu mkuu wa mamlaka ya dawa za asili nchini China alisema mwezi Machi.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO