Takwimu zilizotolewa na chuo kikuu cha Johns Hopkins zinaonyesha kwamba vifo katika mataifa ya Marekani ,Brazil na India vinajumuisha nusu ya vifo vyote duniani .
Wataalam wanaonya kwamba idadi kamili huenda iko juu Zaidi .katibu mkuu wa umoja wa mataifa António Guterres amesema idadi hio ni kuhofisha
" Walioaga dunia walikuwa baba ,mama ,dada ,kaka wake na waume ,marafiki na wenzuru . uchungu wa kuwapoteza umezidishwa na makali ya janga hili’ amesema Guterres
Hatua hiyo imejiri miezi kumi tangu ugonjwa huo kulipukia nchini China katika mkoa wa Wuhan .
Janga hilo limesambaa hadi katika mataifa 188 huku visa milioni 32 vikithibitishwa . hatua za kuzuia maambukizi Zaidi kama vile marufuku za kutotoka nje na kutosafiri zimesababisha chumi za mataifa mengi kudhoofika .
Kwingineko juhudi za kutafuta chanjo dhidi ya coronavirus zinaendelea ingawaje shirika la afya duniani WHO limesema kwamba ugonjwa huo huenda ukasababisha vifo vya watu miliopni 2 kabla ya chanjo kamili kupatikana .
Marekani ndio yenye idadi kubwa ya watu walioaga dunia baada ya watu Zaidi ya 205,000 kuangamia ikifuatwa na Brazil ikiwa na watu 141,700 kisha india ni ya tatu kwa vifo 95,000