Akizungumza kuhusu mikakati iliyochukuliwa na sekta ya kifedha kupambana na usambaaji wa virusi hivyo gavana wa benki kuu Patrick Njoroge amewarai wananchi kutumia fursa ya kuondolewa kwa ada za kutuma pesa za malipo wanapofanya ununuzi badala ya kutumia pesa taslimu. Sekta ya beki imekubali kulegeza mashari kuhusu mikopo hasa iliyochukuliwa na watu binafsi kuhakikisha kwamba watu wanamudu kugharamia mahitaji yao ya kila siku .
'' Mikopo yote ya Benki iliyokuwepo machi tarehe mbili itaweza kuongezwa muda wa malipo hadi mwaka mmoja . wafanyibiashara wadogo wadogo na mashirika yanaweza kuzungumza na benki zao kuhusu kuongezwa muda wa malipo kulingana na Njoroge .
“ Pia tumezitaka benki zetu kuodnoa ada za kufahamu masalio ya pesa katika kaunti na hawafai kutoza malipo yanayotekelezwa kutumia kumbi za simu za mkononi’ ameongeza Njoroge .
Mwenyekiti wa muungano wa wanabenki wa Kenya na maneja mkurugenzi mkuu wa benki ya KCB Joshua Oigara amekariri kujitolea kwa sekta ya benki kuwasaidia wakenya kukabiliana na virusi vya COVID 19 nchini