COVID-19: Mtu na mkewe waruhusiwa kwenda nyumbani licha ya kupatikana na virusi vya Corona

Kagwe
Kagwe
  Kwa mara ya kwanza  serikali imewaruhusu mtu na mkewe waliopatikana na vitusi vya Corona kwenda nyumbani ili kupona

Wawili hao waliwasili Nairobi tarehe tano mwezi huu   na wameruhusiwa kwenda nyumbani katika mtaa wa Kitisuru na kujitenga kwa siku 14. Wawili pamoja na raia mmoja wa Burundi  ndio waliosajili visa vitatu vya hivi punde vya ugonjwa huo . Raia huyo wa Burundi hata hivyo ametengwa katika hospitali ya Mbagathi .

Visa hivyo vipya vitatu sasa vimefikisha jumla ya visa saba vya watu waliopatikana na virusi vya Corona  nchini  baada ya kisa cha kwanza kuripotiwa Ijumaa wiki jana . Afisa mmoja kutoka wizara ya afya amesema wanandoa hao walifaulu kuwathibitishia kwamba wangeweza kujitenga wakiwa nyumbani kwao na hivyo basi kuruhusiwa kwenda .