Brenda Cherotich na Brian
Brenda Cherotich na Brian ni miongoni mwa watu watatu nchini Kenya ambao wamepona virusi vya Corona .Wawili hao siku ya Jumatano walizungumza na rais Uhuru Kenyatta kupitia njia ya video na kulitangazia taifa jinsi walivyojipata na virusi hivyo na muda wao katika karantini. Brenda alieleza jinsi ugonjwa huo unavyoweza kukabiliwa na kuwahimiza wakenya walio na daalili za virusi vya Corona kuwa na ujasiri wa kujitokeza mapema ili kupata usaidizi wa matibabu .
Mwana FA
Mwanamuziki huyo wa bongo aliwashangaza mashabiki wake kwa kutangaza kupitia instagram kwamba alikuwa amepatikana na virusi vya Corona . Alijitega katika karanti kwa muda alioshauriwa na madaktari na baadaye akatangaza kupona . Waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu alithibitisha kwamba Mwana FA ndiye aliyekuwa mgonjwa wa kwanza nchini humo kupona virusi vya COVID 19 .
Salaam SK
Maneja huyo wa msanii wa Bongo Diamond Platinumz alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliopatikana na virusi vya Covid 19 . Tangazo kwamba Salaam alikuwa na virusi hivyo lilimpelekea Diamond pia kuingia karantini ili kujitenga na uwezekano wa kuambukizwa. Baadaye hata hivyo Salaama aliibuka na habari njema kwamba ameweza kupona virusi vya Corona .