Mercy Mwangangi

Covid-19: Visa vya maambukizi ya corona vyafika 36,393 baada ya watu 92 kupatikana na corona

Kenya hii leo imesajili visa 92 vya maambukizi ya corona na kufikisha idadi ya 36,393 kutokana na sampuli 2,985 zilizopimwa kati ya saa 24 zilizopita, amesema katibu msimamizi wa wizara ya afya  Mercy Mwangangi.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 75, kutokana na maambukizi hayo mapya, 64 ni wanaume na 28 wakiwa wanawake.

Covid-19: Watu 10 waaga dunia huku 96 wakipatikana na corona

Pia kati ya maambukizi hayo wote ni wakenya ilhali wanne ni raia wa kigeni.

Huku hayo yakijiri, watu 165 wamepona kutokana na maambukizi hayo, huku 105 wakipona baada ya kupokea matibabu hospitalini na 60 katika mpango wa utunzi na matibabu ya nyumbani.

covid-19: Watu 176 wamepona corona huku 48 wakipatikana na virusi hivyo

Hii leo watu 3 wamepoteza maisha yao na kufikisha idadi jumla ya 637 ya watu walioaga dunia kutokana na virusi hivyo

Photo Credits: radiojambo

Read More:

Comments

comments