Kenya leo imesajili visa 183 vya virusi vya corona na kufikisha visa hivyo kuwa 8,250 katika saa 24 zilizopita. Matokeo hayo ni kutoka sampuli 2,061 amesema waziri wa afya Mutahi Kagwe.
Kutoka visa hivyo 177 ni vya wakenya ilhali sita ni vya raia wa kigeni . watu 119 ni wanaume ilhali 64 ni wanawake huku mtu mwenye umri wa chini sasa akiwa na umri wa miaka minne na aliye na umri wa juu zaidi akiwa na umri wa miaka 64 .
Nairobi inaongoza kwa visa 100 ,machakos ikiwa na visa 37 ,kiambu ina visa 14 ,Mombasa ina visa 13 ,Kajiado visa 11 ,Nakuru visa 5 na Busia ina visa 3.
Wagonjwa 90 wameruhusiwa kwenda nyumbani na kufikisha 2504 watu waliopona ugonjwa huo huku watu watatu wakiaga dunia na kufikisha 167 waliofariki kutokana na ugonjwa huo .
Waziri Kagwe amewaonya wakenya dhidi ya kuwa watepetevu hasa baada ya rais Uhuru Kenyatta kufungua usafiri kutoka kaunti moja hadi nyingine .
Rais Kenyatta hata hivyo alizidisha muda wa kafyu kwa siku 30 zaidi .