Covid-19: Watu 136 wapatikana na corona huku 99 wakipona

Watu 136 hii leo wamepatikana na maambukizi ya corona na kufikisha idadi ya jumla 35,020, hii ni baada ya sampuli 3,707 kupimwa kati ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 85 ni wanaume huku 5i wakiwa wanawake, pia 124 ni wakenya ilhali 12 ni raia wa nchi ya kigeni, mgonjwa umri wa chini ana miezi tisa na mwenye umri wa juu ana miaka 75.

Hayo yakijiri watu,99, wamepona kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 21,158 waliopona maambukizi ya corona tangu kisha cha kwanza kutipotiwa.

Vilevile watu 5 wamepoteza maisha ya kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 594 walioaga kutokana na corona, Mungu azilaze roho zao mahali pema.