Covid-19: Watu 781 wamepona huku 699 wakipatikana na virusi vya corona

Watu 781 wameruhusiwa kuenda nyumbani baada ya kupona virusi vya corona huku idadi ya waliopona ikifika 11,899watu waliopona, haya yakijiri watu,699 wamepatikana na virusi vya corona na idadi kufika 25,837 ya watu walioambukizwa virusi hivyo.

Hii ni kutokana na sampuli 7,175 zilizopimwa chini ya saa 24, wagonjwa 427 ni wanaume bali 272 ni wanawake amesema waziei wa afya Mutahi Kagwe.

Hii leo watu 5 wamepoteza maisha yao kutokana na virusi vya corona na kufikisha idadi ya jumla 418 ya watu walioaga kutokana na corona.

Akizungumza akiwa katika kaunti a Kakamega Mutahi amesema kuwa mgonjwa wa umri wa chini ana mwaka mmoja na huku aliye na umri wa juu akiwa ana miaka 89.

Pia alimpongeza gavana Wycliffe OParanya kwa kazi yake nzuri, alioifanya kwa kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya corona.