COVID 19:Maafisa watatu wa polisi Kamukunji wapatikana na coronavirus

kamukunji
kamukunji
Polisi  katika kituo cha polisi cha Kamukunji  watafanyiwa vipimo vya covid 19 baada ya wenzak watatu kupatikana na ugonjwa huo .

Kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kiliripotiwa baada ya  polisi mmoja kupatikana na ugonjwa huo baada ya kupimwa katika hospitali ya Ag Khan siku ya ijumaa . Afisa  huyo amejitenga nyumbani kwake Ruiru akifanyia matibabu na chini ya uangalizi wa madaktari .

Afisa  mwingine wa cheo cha Constable  kutoka kituo hicho  anayehudumu katika kundi la  kushughulikia dharura za matibabu katika chuo cha mafunzo ya DCI South C pia alipatikana na ugonjwa huo  na kupoelekwa katika  hospitali ya rufaa na mafunzo ya chuo kikuu cha Kenyatta .

Familia yake imetengwa katika nyumba yao  katika nyumba za polisi mtaani kamukunji .

Afisa wa tatu ni mkaazi wa mtaa wa  Fuata Nyayo  aliyepatikana na virusi hivyo baada ya kupimwa katika hospitali ya  Mbagathi  siku ya ijumaa .

Siku ya ijumaa Kenya ilisajili visa 117  vya ugonjwa huo na kufikisha jumla ya  4,374.

Wizara ya afya  imezidi kuwatahadharisha wakenya dhidi ya kupuuza maagizo inayotoa ili kupambana na usambaaji wa covid 19  baada ya watu wengi kuanza kurejelea shughuli zao za kawaida bila kuzingatia  maelekezo yote yaliyotolewa hapo awali

Wakati huo huo shughuli za mahakama katika kaunti ya Mombasa zimesitishwa baada ya  maafisa 11 wa  idara ya mahakama kupatikana na ugonjwa huo .