covid-19:Watu 105 wapatikana na corona huku kukiwa hamna visa vya vifo

Kenya hii leo imesajili visa 105 vipya vya maambukizi ya corona na kufikisha idadi jumla ya 36,829  vya watu walioambukizwa corona hii ni kutokana na sampuli 2,868 zilizopimwa ndani ya saa 24.

Huyu haya yakijiri waziri wa wizara ya afya Mutahi Kagwe ametangaza kuwa kati ya maambukizi hayo mapya 83 ni wanaume huku 22 wakiwa na wanawake.

Pia mgonjwa mwenye umri wa chini ana miaka miwili huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 95.

Hii leo watu68 wamepona kutookana na virusi vya corona na kufikisha idadi jumla ya 23,777 waliopona kutokana na corona huku 38 wakiwa wamepona wakipokea matibabu ya nyumbani na 30 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospotali tofauti.