Covid-19:Watu 179 wamepatikana na virusi vya corona

Kenya imesajili visa 179 vipya vya maambukizi ya virusi vya corona na kufikisha idadi ya  34,884 hii ni kutokana na sampuli 4178 zilizopimwa saa 24 zilizopita.

Katibu mratibu wa wizara ya afya Rashid Aman amesema kuwa  wananchi wasilege kamba ya kuzuia maambukizi ya corona alizungumza haya akiwa katika kaunti ya Bomet huku kaunti hiyo ikifikisha jumla ya watu 22 walioambukizwa na virusi hivyo.

Vile vile watu 4 wamepoteza maisha yao na kufikisha idadi ya 589 ya watu wakioaga kutokana na virusi hivyo amesema Rashid Aman.

Pia watu 415 wamepona na kufikisha idadi ya 21,059 waliopona kutokana na virusi vya corona.