Covid-19:Watu 473 wapatikana na corona na kufikisha visa hivyo kuwa 9448 nchini

Kenya leo imesajili visa vingi zaidi vya watu walio na ugonjwa wa corona kwa siku moja baada ya watu 473  kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo na kufikisha jumla ya wagonjwa wa corona kuwa 9448.

Idadi hiyo ndio ya juu zaidi tangu kutangazwa kwa kisa cha kwanza cha virusi vya corona Machi mwaka huu, katika visa hivyo 324 ni vya wanaume na 149 ni vya wanawake.

Mtoto wa mwaka mmoja ni miongon mwa walioambukizwa visa hivyo, Wagonjwa 76 wameruhusiwa kwenda nyumbani na  kufikisha  watu 2733 waliopona ugonjwa huo.

Akizungumzia katika kaunti ya Kilifi waziri Kagwe amewasifu maafisa wa kaunyi hiyo hasa gavana wa kaunti ya kilifi kwa mikakati waliochukua kuzuia maambukizi ya virusi hivyo.

Pia wagonjwa nane wameweza kufariki kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi ya waliofariki 181 kutokana na ugonjwa huo,kaunti hiyo ina visa 78 huku leo ikisajili visa 3.