Covid-19:Watu 492 wapatikana na virusi vya corona

Kenya hii leo imerekodi visa 492 vipya vya maambukizi ya corona, na kufikisha idadi ya jumla 26,928 ya watu walioambukizwa virusi hivyo hii ni kutokana na sampuli 4063 zilizopimwa chini ya saa 24.

Watu 534 wamepona kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 13,495 ya watu waliopona virusi vya corona Mutahi Kagwe alisema.

Kaunti ya Nairobi inazidi kuongoza kwa maabukizi hayo huku hii leo ikifuatwa na kaunti ya Garissa, huku haya yakijiri watu wengine watatu wameaga dunia kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi ya jumla 423 ya watu walioaga dunia kwa ajili ya virusi vya corona.

Huku akizungumza alisema kuwa hospitali zinapaswa kuzingatia kupeana ripoti zifaazo za maambukizi ya corona, pia alisema kuwa mgonjwa wa umri wa chini ana miezi kumi na moja na wa juu ana miaka 83.