Covid-19:Watu 723 wapatikana na virusi vya corona huku 16 wakifariki

Mutahi Kagwe
Mutahi Kagwe
Watu 723 wamepatikana na virusi vya corona huku idadi ya maambukizi ya virusi hivyo ikifika 20,636, Visa hivyo vipya  vimetokana na sampuli 8,679 ambazo zilipimwa katika kipindi cha  saa 24 zilizopita .

Katka visa hivyo vipya watu 450 ni wanaume na 273 ni wanawake, kulingana na miaka aliye na umri wa chini ni mtoto wa miezi tisa na umri wa juu ni mgonjwa wa miaka 87.

Haya yakijiri watu,16, wamefariki kutokana na virusi hivyo na idadi hiyo kufika 341, pia watu 44, wameruhusiwa kueenda nyumbani na kufikisha idadi ya waliopona 8165 waziri wa afya Mutahi Kagwe alisema.

Pia aliwatakia Waislamu wote sikukuu njema,huku akiwashauri wazingatie amri na maagizo ya wizara ya afya wakati huu wanasherehekea.

Mutahi alisema kati ya walioaga dunia leo, kuna mwanamke wa miaka 22, ambaye aliaga akiwa kwenye hospitali kuu ya Kenyatta huku kumi walioaga ni wa kutoka katika hospitali ya Kiambu ya level five.