Covid 19: WHO yasema hali ya maambukizi itakuwa mbaya zaidi siku zijazo

WHO
WHO
Kuna uwezekano wa hali kuwa  mbaya zaidi wakati huu wa janga la Covid-19, Shirika la afya duniani (who) limetahadharisha, miezi sita ikiwa imepita tangu mlipuko wa ugonjwa huo kutokea.

Mkuu wa shirika hilo, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema virusi vinaweza kuathiri watu wengi zaidi ikiwa serikali hazikuanza kutekeleza sera sahihi.

Ujumbe wake ulibaki kuwa ''Pima, fuatilia, tenga na weka karantini'', alisema.

Zaidi ya watu milioni 10 wamethibitishwa kuwa na maambukizi duniani tangu virusi hivyo vilipojitokeza nchini China mwishoni mwa mwaka jana.

Idadi ya wagonjwa waliopoteza maisha sasa ni zaidi ya 500,000

Nusu ya idadi ya watu walioambukizwa duniani imekuwa Marekanni na Ulaya, lakini idadi inaongezeka kwa kasi Amerika.

Virusi hivyo pia vinaathiri Kusini mwa Asia na Afrika, ambako hakutarajiwi ongezeko la juu mpaka mwishoni mwa mwezi Julai.

Dkt Tedros akitoa hotuba yake siku ya Jumatatu alisema: ''Sote tunataka hali hii kuisha. Sote tunataka kuendelea na maisha yetu. Lakini ukweli ulio mchungu ni kuwa bado hali hii haijafikia kuisha hata kidodo''

'' ingawa nchi nyingi zimepiga hatua, bado ugonjwa huu unashika kasi duniani.''

''Kukiwa na wagonjwa milioni 10 sasa na vifo vya watu nusu milioni, mpaka pale matatizo yaliyogundulika yatakajulikana na WHO, ukosefu wa umoja wa kitaifa na kidunia na dunia iliyogawanyika hali inayosaidia kusambaa kwa virusi…bado hali itakuja kuwa mbaya zaidi,'' alisema.

''Samahani kwa kusema hivyo, lakini kwa mazingira ya namna na hali hii, tunahofu hali kuwa mbaya .''

Amezitaka serikali kufuata mifano ya Ujerumani, Korea Kusini na Japan, ambazo zimekuwa zikichukua hatua kudhibiti maambukizi kwa kutumia sera ikiwemo vipimo na ufuatiliaji.

Marekani imeripoti kuwa na watu milioni 2.5 walioathirika na vifo karibu 126,000 vilivyotokana na Covid-19 mpaka sasa- zaidi ya taifa jingine lolote.

Majimbo ya nchini Marekani katika wiki za hivi karibuni- hasa kusini yameripoti ongezeko la maambukizi mapya.

Ongezeko hilo limefanya maafisa wa Texas, Florida na majimbo mengine kuweka mazuio makali tena kwenye biashara.

Nchi ya pili iliyo na kiasi kikubwa cha maambukizi ni Brazil, iiwa na watu walioambukizwa milioni 1.3 na vifo zaidi ya watu 57,000.

Siku ya Jumatatu hali ya dharura ilitangazwa katika mji mkuu Brisilia, kutokana na ongezeko la maambukizi.