Covid19;Wahudumu wa afya wataka wenzao wa umri wa juu kupewa likizo

Miunguno ya wahudumu wa afya sasa inataka wanachama wake wa zaidi ya umri wa miaka 55 kupewa likizo hadi pale janga la coronavirus litakapokuwa limedhibitiwa.

Katika matakwa yao kwa kongamano la leo linaloongozwa na rais Uhuru Kenyatta kutathmini mikakati ya kukabili maambukizi ya virusi vya corona, maafisa wa miungano yao pia wanataka serikali kuajiri zaidi ya wahudumu 10,000 kujaza pengo la wale wanaoambukizwa virusi ili kushughulikia idadi kubwa ya maambukizi inayosajiliwa nchini kila kuchao.

Soma pia;

Viongozi wa miungano hiyo wakizungumza siku ya Jumapili mjini Nairobi, walisema kwamba wahudumu wa ziada watafanikisha shughuli ya kuwapa huduma muhimu watu wenye mahitaji maalum ili kuwakinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Taarifa hiyo ilitolewa na viongozi kutoka miungano ya  maafisa wa utabibu (Clinical officers) wauguzi, maafisa wa maabara, wanafamasia, wataalam wa afya na wataalam wa lishe.

Soma pia;

Viongozi wa miungano hiyo wakizungumza siku ya Jumapili mjini Nairobi, walisema kwamba wahudumu wa ziada watafanikisha shughuli ya kuwapa huduma muhimu watu wenye mahitaji maalum ili kuwakinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Walisema kwamba jumla ya wahudumu wa afya 531 wameambukizwa virusi vya corona kufikia sasa wakiwa kazini huku saba kati yao wakifariki kutokana na maradhi ya covid-19.

“Huku kongamano hilo likifanyika, tungependa wajuwe kuwepo kwa changamoto hizi kwa sababu hicho ndicho kitengo cha juu zaidi katika kufanya maamuzi nchini Kenya. Tunawasihi wazingatiye changamoto hizi na kuzipa kipao mbele ili kuhakikisha kwamba mahitaji yetu yanatiliwa maanani tunapokabiliana na virusi hivi,” Katibu mkuu wa muungano wa maafisa wa utabibu George Gibore alisema.

Miungano hiyo ilifanya utafiti kati ya Julai 23 na 25 kubaini mikakati ya kuzuia maambukizi ya virusi hivyo miongoni mwa wahudumu wa afya katika taasisi za umma na kibinafsi.

Utafiti huo ulibaini kwamba ni asilimia 24.9 pekee ya wahudumu wa afya waliopokea mafunzo ya siku mbili kuhusu covid-19.

Soma pia;

Kulingana na utafiti huo pia, asilimia 72.5 ya maafisa wa afya wanaoendesha zoezi la kupima wananchi hawana magwanda yanayohitajika kwa zoezi hilo na hawana maski aina ya N95. Asilimia 74.4 hawana uhakika ikiwa wanatumia vifaa hivyo kama inavyotakikana.

“Hii inaeleza ongezeko kubwa la maambukizi miongoni mwa wahudumu wa afya,” Gibore alisema.

Asilimia 64.5 waliripoti kuhisi uchovu kutokana na kazi nyingi huku asilimia 82.4 wakihisi kuwa mshahara wao hauambatani na kiwango cha hatari wanayokabiliana nayo wakiwa kazini.