Crime Alert: Mke wa jeshi abakwa na kuuawa Busia

Maafisa wa polisi mjini Webuye wanawazuilia watu wawili wanaoshukiwa kumbaka na kumuua mwanamke mmoja wa miaka thelathini ambaye ni mkewe afisa wa KDF eneo la Hurlingham  jijini Nairobi.

Martha Musundi mama wa motto mmoja alipatikana mapema leo akiwa amefariki chumbani mwake bila majeraha yeyote.

Mzee wa kijiji wa eneo hilo Japheth Soita amesema kwamba washukiwa wawli hao walipatikana na simu, kikoi na begi ya marehemu.

Mwili wa mwendazke umepelekwa katika hifadhi maiti ya hospitali ya webuye huku uchunguzi zaidi ukiendelea.