Suicide

Crime News: Mwanafunzi wa darasa la tano ajiuuwa

Hali ya huzuni imekubika familia moja kutoka kijiji cha Shaviringa ndogo ya makuchi kaunti ndogo ya Hamisi baada ya mvulana wao wa miaka 13 kujitoa uhai kwa kujinyonga na kamba.

Akithibitisha tukio hilo, chifu wa kata ya Shiru josephine Khalwale amesema kuwa mvulana huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano alichukuwa kitu kutoka kwa kibanda cha jirani na mmiliki alipomshitaki kwa wazazi aliathibiwa kwa kosa hilo na akatoeka.

Wazazi wake walianza kumtafuta jioni na kugundua saa nne unusu za usiku mwili wake umeninginia kwenye nyumba moja ambayo hakuna anayeishi humo ndani.

Mwili wa marehemu uliondolewa na kufikishwa chumba cha wafu cha hospitali ya rufaa ya Vihiga.

Photo Credits: file

Read More:

Comments

comments