Akiwa na umri wa miaka 24 wakati huo nchini Australia akisomea Sheria ,Nduku alikutana chuoni na mkenya mwenzake ,kijana mtanashati sana na mpole kutoka Ukwala ,Siaya . Iwapo umewahi kuishi nje ya Kenya unaweza kufahamu hisia hii ya kuwa mbali na nyumbani kasha ukutane na mtu ambaye yuatoka Kenya .Ni jambo zuri san aka sababu mnaweza kuzungumza mengi kwa wakati mmoja ikaonekana ni kana kwamba mmejuana maisha yenu yote .Hivyo ndivyo ilivyokuwa kati ya Nduku na Derick Ochola.‘Kila kitu kilikuwa sawa tulipokutana na nilijua kuanzia mwanzo kwamba huyu diye ninayemtaka kama mpenzi wa muda mrefu’. Anasema Nduku . Ochola naye hakuchelewa kwani baada ya kukutana hapa na pale chuoni alimtaka waweze kupatana pia nje ya chuo ,na ikawa rasmi kwamba walikuwa wanapendana hivyo basi shughuli zao nyingi wakawa wanazifanya pamoja . Alipowajulisha jamaa zake wakati wa likizo kwamba amekutana na mkenya mwenzake ambaye wamependana na wanapanga kufunga ndoa baada ya masomo yao ,familia nzima ilijawa furaha na kweli wakati huo kila kizuri cha maisha kilionekana!
Baada ya miaka miwili ambapo wote sasa walikuwa wamemaliza kusoma na kupata kazi ,walikubaliana kurejea Kenya ingawa kwa muda kidogo Nduku alibaki Australia . walifunga ndoa ya kanisani wakiwa ng’ambo nan i jamaa zao wachache ndio walioweza kuishuhudia ndoa hiyo ingawaka walituma picha na kanda za video kwa wengi wa waliokuwa Kenya wakati huo . Ilikubaliana kwamba wangefanya harusi nyingine wakiwa Kenya na pia kufuatilizia na hafla ya kitamaduni ili kuashiria sasa kwamba wamekuwa mke na mume na hayo yakafanyika wakati wote walipokuja Kenya .
Kwa bahati mbaya miezi sita tangu waje Kenya kuishi na kuanza familia yao nyumbani ,Ocholla alihusika katika ajali ya barabarani wakati gari alilokuwa akiendesha kugongana na trela kwenye barabara kuu ya Nairobi kwenda nakuru na ilikuwa kipindi cha pasaka 2016. Nduku hakujua kuhusu kifo cha mumewe hadi alipoona kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuna watu waliofariki kwenye ajali iliyotokea eneo la kabati .Kilichomshika jicho ni rangi ya mojawapo ya magari yaliyohusika kwenye ajali hiyo-gari dogo jekundu..na kwa hofu yake akaiangalia picha ile kwa karibu ili kuona nambari ya usajili na hapo ndipi ulimwengu wake ulizima kwa dakika kama tano.Hakuweza kupumua waka kuzungumza na akasalia kama bubu asijue cha kufanya . Alipopata ujasiri kitu cha kwanza alichofanya ni kmpigia mume wake simu lakini haikukereza kwani alikuwa mteja.
Hakuhitaji tena ufafanuzi kwamba alikuwa mjane .mume wake alikuwa ashafariki na hilo likathibitishwa na shemeji yake ,kakake mumewe ambaye alimpigiasimu akimueleza anakuja kumchukua hadi Nakuru wautambue mwili kasha matayarisho ya kumzika yaanze.Safari ya huzini ,simanzi na mshangao ilikuwa ndio imeanza kwa Nduku. Kwa ufupi ,kando na kuomboleza kifo cha mumewe kabla ya maazishi Nduku aliarifiwa kuhusu mila za watu wa akina mumewe na hakuelewa kilichokuwa kikifanyika hadi mkesha wa kuzikwa kwa Ocholla. Nduku aliambiwa kwamba atalala katika chumba kimoja na mwili wa mume wake na wakati wa mchakato huo ,anafaa kupata ndoto ya kushiriki tendo la ndoa naye.Maskini mtoto kutoka Matuu ,alishangaa ,akashindwa la kufanya lakini kaambiwa huo ni utamaduni wa jamii ya Waluo . Siku za jadi wajane katika jamii hiyo walitakiwa kufanya hivyo kabla ya waume zao kuzikwa ili ‘wasafishwe’ kwa matayarisho ya kurithiwa.
‘Niliambiwa kwamba endapo ningepata ndoto ya kushiriki tendo la ndoa na mume wangu kabla hajazikwa basi ningekuwa huru na tayari kuolewa tena’ anasena Nduku .
Anaongeza ‘ Iwapo ndoto haingekuja basi njia nyingine ya tambiko ingetumiwa ili kunifanya niwe ‘msafi’ kabla ya maazishi’
Ili kufupisha masimulizi yake ,hakuna aliyemtayarisha Nduku kwa yote yaliomfika kuanzia kifo cha mume wake na utamaduni wa watu wake.Alipokuwa hai alikuwa akimdokezea baadhi ya mila hizo lakini kwa sababu alikuwa msomi ,Ocholla hakuwa akizipa uzito sana mila za watu wa jamii yake lakini palipo na wazee ,utamaduni hausahaulikwi hivi hivi .Je,ni zipi mila za jamii nyingine ambazo kwako umeziona kuwa na kushangaza? Ungefanya nini iwapo unhejipata katika hali ya Nduku?