SONKO

D–DAY:Sonko kufikishwa kortini Voi kwa kumshambulia afisa wa polisi .

Gavana wa Nairobi Mike Sonko  atafikishwa kortini  leo  huko Voi  ili kujibu mashtaka ya kumshambulia  afisa mmoja wa polisi . Gavana huyo alifikishwa  kortini disemba tarehe 18  mwaka jana  mbele ya hakimu mkaazi Fredrick Nyakundi  lakini mawakili wake walisema hakuwa katika hali nzuri kujibu mashtaka na alihitaji kupumzika . Siku ya jumatatu  wakili wa Sonko Cecil Miller  alisema mteja wake  atakuwa kortini .

 

Kenya Ina Mambo! Video ya Jamaa mmoja akipiga punyeto hadharani yawashangaza wanamitandao

Stakabadhi ya mashtaka inasema Sonko alimshambulia afisa mmoja mkuu wa polisi mweno saa sita unusu  wakati polisi huyo alipokuwa akitekeleza kazi yake  kinyume na  ibara ya 103 ya sharia ya huduma ya polisi ya mwaka wa 2011 . Sonko ameshtumiwa kwa kumpiga teke  kamanda wa polisi wa eneo la pwani Rashid  Yakubu katika uwanja mdogo wa ndege wa Ikanga .

DISARMED AND HOPLESS: Wafahamu Viongozi 7 watakaopokonywa ulinzi wa polisi na Bunduki .

Mashahidi wanne  akiwemo Yakubu na maafisa wa polisi James Mwanzia, Michael Muriithi,  Fred Sabai, Stephen Mtawa na Ibrahim Ahmed  wameorodheshwa kutoa ushahidi dhidi ya Sonko . Kisa hicho kilitokea Disemba tarehe sita  wakati gavana huyo alipokuwa akikamatwa k katika kizuizi kimoja cha barabarani ili kujibu mashtaka ya ufisadi City Hall. Sonko anakabiliwa na mashtaka 19 ya ufisadi ,utumiaji mbaya wa maalaka ya afisi yake na malipo yasio halali ya shilingi milioni 357.

 

 

 

Photo Credits: Radio Jambo

Read More:

Comments

comments