akothee

Daah! Akothee azua balaa bungeni kwa kuvaa nguo fupi

Mwanamziki stadi Akothee, alizua vurugu siku ya Jumatano baada ya kuenda bungeni na nguo iliyokuwa fupi kupitia kiasi.
Akothee alikuwa amenda bungeni kumsalimia mbunge David Sankok na ndipo walinda lango pamoja na wengi waliokuwa bungeni wakabaki wameduwaa na kumzuia asiingie hoteli iliyo bungeni.
Baada ya vurugu kidogo na wanasheria wa bungeni, Akothee alikubaliwa apite na kuingia bungeni bila walinzi wake.
Zaidi ya hayo, wanasheria wa bungeni walijaribu kumpa kikoi ajifunge lakini mipango yao ikaambulia patupu. Akothee alikuwa amevalia mini sketi ya rangi ya kijani ambayo haikuwa karibu hata kufika magotini.
akothee
Baada ya dakika chache za kubishana na wanasheria wa bungeni, Akothe alipewa ruhusa na kuambiwa atumie mlango wa nyuma kuingia kwenye hoteli hiyo ya bungeni.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments